Mpira wa miguu unapanga yake Mwenyezi Mungu anapanga yake ishi na watu vizuri kwasababu kesho haileweki unaweza kuwa rafiki wa kifo,fainali inaweza kuwa rafiki wa ndoa.Kabla timu yako haijacheza fainali kabla kifo hakijakufika inua mikono juu muombe Mwenyezi Mungu akupe mwisho mwema.
Pale Lupaso hakuna tofauti na viwanja vya makaburi, kifo na fainali vibaki kuwa fumbo hatujui kinachoendelea kuhusu wafu pia hatujui tarehe 28 huzuni itakuwa upande wa kaskazini au kusini na labda furaha itaondoka kwenye mioyo ya mashabiki wa jangwani.
Basi tarehe 28 kabla haijafika muombe Mwenyezi Mungu akupe busara usimcheke jirani yako kwasababu fainali ni kifo na makaburi hatujui yatatuchukua lini tukalale usingizi wa milele pale Lupaso.
Ameandika Omar Kombo