Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fainali Ngao ya Jamii Yanga vs Simba kiingilio Tsh 20,000

Yanga Day Pic Mashabiki wa Yanga

Sat, 12 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa fainali ya ngao ya jamii kati ya Yanga Sc na watani wao wa jadi, Simba SC utakaochezwa kesho Jumapili, Agosti 13, 2023 katika Dimba la CCM Mkwakwani, Tanga.

Wadau wa michezo walikuwa wakiishauri TFF kupandisha kiingilio ili kuondoa msongamano unaoweza kujitokeza kutokana na uwanja huo kuwa mdogo ikilinganishwa na ukubwa wa mechi husika na wingi wa mashabiki wa timu hizo kongwe na kubwa nchini Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na TFF inaonyesha viingilio titakuwa kama ifuatavyo;

◉ Jukwa la mzunguko - Tsh 20,000 ◉ Jukwaa la VIP B - Tsh 30,000.

Mchezo huo unaozikutanisha timu watani wenye historia kubwa katika soka la Afrika, utapigwa saa 1:00 jioni kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimubwa 2023/24.

Aidha, pesa zitakazopatikana kutokana na makusanyo ya mlangoni ya mchezo huo, zitaelekezwa kwenda kusaidia wenye mahitaji maalum.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: