Wakati Vigogo wa Soka la Tanzania Klabu za Simba na Yanga wakijiandaa kukipiga kesho Jumapili Agosti 13 katika Fainali ya Mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Dabi hiyo inaweka rekodi yake baina ya vigogo hao wawili nchini:
Hii ni Kariakoo Derby ya Kwanza kwa Simba na Yanga kupigwa Mkwakwani, Tanga, lakini ni pambano la tatu mfululizo baina ya timu hizo kukutana baada ya fainali ya Kombe la ASFC 2020-21 iliyochezwa Lake Tanganyika, Kigoma.
Katika mchezo huo Simba ilishinda bao 1-0 kabla ya Yanga kuifumua Simba 1-0 katika nusu fainali ya michuano hiyo jijini Mwanza msimu wa 2021-222.
Tanga imeingia katika historia ya miji iliyoshuhudia Kariakoo Derby miaka tofauti mbali na Dar es Salaam ikifuata nyayo za Mbeya, Arusha, Dodoma, Unguja, Mwanza, Morogoro na Kigoma kwa mechi mbalimbali zikiwamo za Ligi Kuu Bara, Kombe la Mapinduzi, ASFC na Kombe la Kagame.
Huu ni mchezo wa tatu wa Ngao kupigwa mkoani kwa misimu ya karibuni baada ya ule wa 2018-2019 kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliopigwa jijini Mwanza, kisha 2020-2021 uliochezwa mjini Lindi na Simba kuitambia Namungo kwa 2-0.
Kadhalika hii derby ya kwanza kwa Simba na Yanga katika msimu huu, lakini ni mechi ya pili mwaka huu wa 2023 baada ya ile ya mwisho ya Ligi Kuu ambapo Yanga ilikandwa bao 2-0.