Hatimaye imejulikana, ni vita ya Mwanaume dhidi ya Mvulana aliyekoma yaani Lionel Messi dhidi ya Mbappe ni baada ya hapo jana Mabingwa watetezi wa kombe la Dunia kureje tena Fainal kwa mara ya pili mtawalia.
Ufaransa ambao ndio Mabingwa watetezi wakitwaa taji hilo 2018 pale Urusi sasa wanalitaka tena baada ya kuwaondosha Morocco katika hatua ya Nusu Fainali kwa mabao (2-0).
Wakati Argentina wao waliwazima Croatia kwa mabao (3-0) hapo juzi, sasa nani kutwaa mwali jumapili hii? Ni vita ya Mwanaume dhidi ya Mvulana aliyekomaa.
Licha ya ubora wa Morocco Ufaransa wanajua jinsi ya kutumia nafasi zao , walipiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango na yote yakazama nyuni , na wanajua kucheza kitimu hasa wakiwa hawana mpira.
Bila mpira Ufaransa wanakuwa umbo la 4-5-1 , tena ni Giroud ndio anarudi mpaka karibu na Griezman na kumuacha Mbappe peke yake mbele tena pembeni ya uwanja mahususi kwa ajili ya mashambulizi ya kushitukiza na ya kujibu, Deschamps akiamini atabaki dhidi ya mabeki wawili tu tena wa kati
Kocha wa Morocco, Regragui aliamua kuanza na mabeki watatu , ili kuwapa athari chanya 'wingbacks' wake ( Hakimi na Mazraoui ) nafasi ya kushambulia zaidi , kuwarudisha nyuma Mbappe na Dembele wakati huo huo kuwapa nafasi nzuri Ziyech na Boufal kushambulia ndani zaidi badala ya kukabiliana dhidi ya Kounde na Hernandez ... mpaka pale Saiss alipoumia
Kipindi cha pili, ndio Morocco walitandaza kandanda safi tangu kuanza haya mashindano hasa wakiwa na mpira ... nini Regragui alifanya ?
Kutengeneza idadi kubwa ya wachezaji pembeni ya uwanja ... kwanini ? Kwasababu Mbappe na Dembele sio wazuri kuzuia kwahiyo Kounde na Hernandez watakuwa wazi sana dhidi ya mikimbio ya Atalah , Boufal na Amallah kushoto , Hakimi Ounahi na Ziyech kulia huku Amrabat anabaki kama namba 6 pekee mbele ya mabeki wawili wa kati
Shida yao ilikuwa Konate na Varane , kila wakipiga krosi Morocco mabeki wawili wa kati wa Ufaransa walikuwa bora sana kwenye kukabiliana nayo.
Hivo ndo fuutiboli ya Dunia huchezwa na timu kubwa Ufaransa wakaibuka washindi kwa ubora wa mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla.
Sasa imebaki michezo miwili kuhitimisha makala ya 22 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930, mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Croatia dhidi ya Morocco na Fainali ya Argentina dhidi ya Ufaransa.