Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fainali Kombe la Dunia: Zamu ya nani leo?

Final Qatar.jpeg Fainali Kombe la Dunia: Argentina vs Ufaransa

Sun, 18 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni Kylian Mbappe au Lionel Messi. Hilo ndilo swali wanalojiuliza wapenda kandanda duniani kote wakati wakisubiri mtangane wa Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia itakayopigwa majira ya saa 12:00 jioni nchini Qatar.

Mchezo huo unaokwenda kupigwa katika Uwanja wa Lusail unazikutanisha timu za Argentina dhidi ya Mabingwa watetezi Ufaransa.

Mchezo huo unavuta hisia za wengi hasa kwa viwango ambavyo vimeoneshwa na timu zote mbili mpaka wanatinga hatua ya Fainali.

Kubwa zaidi dunia inasubiri kumtazama mchezaji bora kuwahi kutokea katika uso wa Dunia Lionel Messi atahitimisha kwa mtindo upi safari yake ya soka kwa upande wa Timu ya Taifa ikizingatiwa Messi baso hajabeba Kombe la Dunia licha ya makubwa aliyoyafanya katika soka.

Messi anakwenda kukumbana na swahiba wake Kylian Mbappe ambae wanakipiga wote katika klabu ya PSG, huku akiwa katika kiwango bora akipeperusha bendera ya Ufaransa.

Mbali na hilo ni vita ya kuwania kiatu cha mfungaji bora ambapo Messi na Mbappe kila mmoja amefunga magoli matano mpaka sasa katika michuano ya mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live