Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fainali AFCON 2027 itapigwa kwa Mkapa - Scanda

Scanda24 1694072433470.jpeg Fainali AFCON 2027 itapigwa kwa Mkapa - Scanda

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa michezo, Biko Scanda amesema Tanzania ina uwezekano mkubwa wa kupata nafasi ya kuandaa sherehe za ufunguzi na mechi ya fainali ya AFCON 2027 kuchezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kwani Kenya hakuna ushawishi mkubwa wa mchezo wa mpira wa miguu katika miaka ya hivi karibuni.

Kingine ni mashabiki ambao wamekuwa hawana mwendeleo mzuri wa kuhudhuria mechi za timu ya Taifa tofauti na walivyofanya wale wa Ivory Coast ambao hawakujali timu yao iko vipi.

“Kule Ivory Coast walifanikiwa kukuza utalii ambao sasa dunia inajua vivutio vinavyopatikana katika nchi yao.

“Wakati Afcon inakaribia walijiandaa kwenye vitu vingi hali iliyoonyesha kuwa wamefanikiwa na kuacha historia.”

Ameongeza katika eneo la wanahabari nao hawakuonyesha ubaya na udhaifu uliopo nchini na badala yake walitangaza mambo mema mengi ya Ivory Coast, jambo ambalo hata sisi tunapaswa kulichukua wakati Shirikisho na wadau wakiendelea kuhakikisha wanaweka mambo sawa katika nyanja zote,” amesema Scanda.

Amesema hayo jana Februari 14, 2024 wakati akichangia mjadala wa Mwananchi Space ulioandaliwa na Mwananchi Communications Ltd, wenye mada isemayo "Tanzania imejifunza nini kupitia AFCON 2023, ikijiandaa 2027?"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live