Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faida za Chama, Miquissone kutamba Afrika

Luis Chama Data Faida za Chama, Miquissone kutamba Afrika

Sun, 11 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ushiriki wa Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu umekuwa ni wa kipekee na sasa hivi imejipambanua kuwa na progressive plans na graph yao inakwenda juu.

Sio tu matokeo pekee bali pia ukiangalia kiwango cha timu uwanjani, wana uniformity play.

Tumeshuhudia wachezaji wake wakichaguliwa katika vikosi bora vya wiki vya Ligi ya Mabingwa ambavyo vinatangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na hii inaashiria kwamba mchango wao ni mkubwa na wamekuwa na muendelezo wa kufanya vizuri.

Hii sio mara ya kwanza kwa wachezaji wa timu za Tanzania kuwahi kuingia katika vikosi kama hivyo kwani hapo nyuma tuliwahi kuingiza wachezaji kama Omary Mahadhi ‘na Maulid Dilunga pindi walipokuwa wakichezea Taifa Stars.

Lakini pia ukiondoa kuchaguliwa katika vikosi bora vya wiki, tumeshuhudia pia Luis Miquissone na Clatous Chama kwa nyakati tofauti wakiibuka wachezaji bora wa wiki wa mashindano hayo.

Luis Miquissone ameteuliwa mara tatu tofauti kuingia katika kikosi bora cha wiki, Chama amefanya hivyo mara mbili wakati Mohamed Hussein na Joash Onyango kila mmoja akiingia mara moja.

Kwa mtu kama Miquissone sio jambo la ajabu kwani amekuwa na muendelezo mzuri wa kufunga katika hatua hiyo ya makundi japo ni ngumu.

Yeye na Chama wamekuwa ni watu ambao wanaonyesha exceptional skills na technically na tactically wako vizuri.

Hilo linapelekea washawishi jopo la ufundi la CAF kuwateua kuingia katika vikosi bora vya wiki na hata kuwa wachezaji bora wa wiki.

Haiji kwa bahati mbaya kwa sababu ikumbukwe wanapigiwa kura na Afrika nzima lakini pia kabla ya hapo kitendo cha majina yao kuingia katika orodha ya wachezaji bora katika mashindano ambayo yanahusisha kundi kubwa la nyota kutoka klabu mbalimbali sio jambo jepesi.

Ziko faida nyingi kwa wachezaji kuteuliwa katika vikosi vya wachezaji bora wa wiki wa mashindano au hata kwa mchezaji mmoja kutangazwa kuwa mchezaji bora wa wiki husika na hapa nitaorodhesha faida saba zinazoweza kupatikana.

Faida ya kwanza ambayo inaweza ni kupatikana ni kuifanya timu iwe na jina kubwa ndani na nje ya nchi. Kila mtu anakuwa anaitaja timu. Kumbuka timu ziko nyingi zinazoshiriki mashindano hayo hivyo wachezaji wale bora wanaochaguliwa ni wachache hivyo wanavyotajwa inakuwa ni rahisi kwa timu kuzidi kufahamika

Nyingine ni kwamba maskauti wanakuwa wanaifuatilia timu kwa ukaribu. Kama timu inatoa wachezaji bora wanaamini kuwa wachezaji wake ni wazuri na faida nyingine ni kwamba kampuni za kibiashara zinakuwa zinavutika kuiona timu na kushawishika kuwekeza na kufanya kazi na Simba zikiamini zitatangazika.

Kampuni hizi zikijitokeza maana yake Simba watapata fedha na zitawasaidia katika kujiendesha.

Faida ya nne ni wachezaji kushawishika kuichezea Simba. Scouts wa Simba hawatopata kazi kubwa katika kuwashawishi nyota mbalimbali kujiunga nao kwa sababu nyuma ya mpira kuna sifa hivyo wachezaji wengi wataona kuwa Simba ndio sehemu wanayoweza kucheza na kupata sifa.

Ukiondoa hilo, pia milango kwa wachezaji wa ndani itafunguka. Timu za nje zinaweza kuja hapa kuchukua wachezaji kwa sababu tayari Simba imesha-attract attention katika maeneo mbalimbali nje na ndani ya bara la Afrika.

Jambo lingine ambalo Simba wanaweza kufaidika nalo ni management na administration kupata maswali ya kujiuliza kwamba tumefanya nini na tukapata faida ambapo kupitia kujiuliza huko wanaweza kutazama mafanikio yao na yakawapa njia sahihi ya kupita ili wazidi kufanya vizuri siku za usoni.

Ni wazi kwamba uongozi wa Simba unafahamu kwamba tayari umeshatengeneza shauku. Umefanya juhudi kuifanya iwe timu kubwa hivyo deni watakalobaki nalo ni kuhakikisha hawarudii makosa ya nyuma kama yalikuwepo na kuweka mikakati bora ya kufanya vizuri mbele.

Ukiondoa hilo pia Simba inanufaika kwa wachezaji wake kujengeka na kupevuka hivyo sasa watakuwa wanaishi kwa misingi ya kiprofessionalism wakiamini kwamba tayari wameshakuwa wachezaji wakubwa na wanatakiwa kuwa kioo na mfano bora kwa wengine.

Mbali na hizo tajwa hapo juu, faida nyingine ambayo inapatikana ni wachezaji kuongezeka thamani na hivyo kuwaweka juu sokoni. Ni jambo lililo wazi kwamba kwa sasa timu nyingine haziwezi kuwaingia kirahisi wachezaji wa Simba ikiwa zinahitaji kuwasajili.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz