Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu sababu za mechi za Ligi Kuu Bara kuchezwa kila siku

Yanga Na Coast Pic Fahamu sababu za mechi za Ligi Kuu Bara kuchezwa kila siku

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inawezekana unajiuliza kwa nini msimu huu 2022|23 mechi za Ligi Kuu zinachezwa karibu wiki nzima? Yaani kila siku kinapigwa!

Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu, Karim Boimanda ametoa ufafanuzi juu ya jambo hilo na kile ambacho kinasababisha mechi za Ligi Kuu kuchezwa karibu kila siku ya wiki.

“Ukiangalia hata kwa wenzetu, kuna ulazima mkubwa wa kufata matakwa au ushauri na maombi ya mdhamini mwenye haki za matangazo ya Television.”

“Tunatamani mechi zote za Ligi Kuu ya NBC zioneshwe mbashara, mdhamini wa haki za matangazo ya Television anatamani kuona mechi zinaoneshwa kwenye channel moja.”

“Mtu akikaa kuangalia mechi kwenye television anaangalia mechi moja ikiisha anaangalia nyingine na sio mechi tatu au nne kuchezwa kwa wakati mmoja kwa sababu kuna watu wengine watakosa kushuhudia baadhi ya mechi.”

“Mdhamini mwenye haki za matangazo ananafasi kubwa sana kwenye hili jambo, ndio maana wamesaidia hata kuweka taa kwenye baadhi ya viwanja ili tuwe na machaguo mengi zaidi ya muda wa kucheza mechi za Ligi.”

“Ni kwa faida ya ukuaji wa Ligi yetu kwamba mechi zote zioneshwe mbashara ili hata mdau wa michezo akiamua kutazama mechi zote za Ligi Kuu awe na hiyo fursa.”

“Kwa hiyo ratiba ya mechi za Ligi kuchezwa karibu kila siku chanzo chake ni kuhakikisha michezo yote inaoneshwa mbashara na mdhamini mwenye haki za matangazo ya television ambaye ni Azam TV.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live