Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu kuhusu wwenza wa Messi, Ronaldo wanavyokula bata

Ronaldo Ret Fahamu kuhusu wwenza wa Messi, Ronaldo wanavyokula bata

Tue, 2 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara nyingi umezoea kuwaona mastaa mbali mbali wa soka Duniani wakiwa wanakula bata kwenye fukwe na kumbi mbali mbali za starehe. Umezoea kuwaona mastaa hao wakisaini madili ya ubalozi wa makampuni mbali mbali makubwa.

Umezoea kuwaona wakiendesha magao ya thamani na kumiliki kampuni za bidhaa mbali mbali.

Lakini upande wapili ni kwamba wale weke zao au wachumba zao pia wana maisha kama hayo kuanzia, bata, mitindo na biashara. Leo tumekuleta wenza wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi jinsi wanavyovaa, wanavyokula bata na maisha yao kijumla.

MITINDO Unajua gharama ya urembo..? Soma hapa sasa. Kawaida Ronaldo anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Pauni 400 milioni ambao utaongezeka zaidi hivi karibuni kutokana na mshahara wa Pauni 174 miloni kwa mwama anaoupata huko Saudi Arabia..

Messi yeye anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Pauni 480 milioni akiwa anakunja jumla ya Pauni 740,000 kwa wiki akiwa na PSG kwa sasa. Utajiri wa wachezaji hawa umewafanya wenza wao wasiwe na mchezo linapokuja suala la urembo kuanzia nguo hadi brandi wanazotumia.

Antonella ameonekana akitumia sana bidhaa za brandi kubwa kama Louis Vuitton, Gucci ana Dolce & Gabbana na amekuwa akionekana mara nyingi kwenye tamasha la Paris Fashion Week tangu Messi ajiunge na PSG.

Mwaka 2021, alionekana amebeba pochi aina ya Louis Vuitton purse ambayo ina thamani ya Pauni 2000 zaidi ya shilingi milioni sita za Kitanzania.

Rodriguez yeye ndio hatari zaidi linaokuja suala hili. Anapendelea zaidi kuvaa gauni la mesmerising Ali Karoui gown linalogharimu zaidi ya shilingi milioni 11 za Kitanzania kulinunua.

Pia huyu ni shabiki wa mabegi ya Hermes' Birkin na anamiliki kibegi cha brandi hiyo lenyewe lina thamani ya , Pauni 146,000 zaidi ya milioni 300 za kibongo.

MIJENGO

Kuishi kwenye sehemu za kifahari ni moja ya mambo ambayo warembo hawa wanayafanya.

Cristiano na Messi wote wamejenga majumba ya kifahari sehemu mbali mbali Duniani.

Messi ametumia zaidi ya Pauni 23 milioni kujenga nyumba maeneo ya Barcelona, Ibiza na Miami.

Wakati Georgina na Ronaldo wanadaiwa kuwa na nyumba yenye thamani ya Pauni 4.8 milioni maeneo ya La Finca huko Hispania, pia wana mjengo wa thamani maeneo ya Turin Italia, mjumba wa kifahari mwingine upo Marbella wenye thamani ya Pauni 1.4 milioni.

Kwa sasa huko Saud Arabia wanaishi jwenye hotel ambayo ina gharimu Pauni 250,000 kwa mwezi ambazo ni zaidi ya milioni 500 za kibongo.

MBELE YA KAMERA Antonella yeye huwa anaonekana kidogo sana pale Messi anapokuwa anafanyiwa mahojiano.

Muda mwingi hupendelea zaidi kuyaweka maish yake binafsi nje ya macho ya watu. Vilevile amekuwa akiwalinda sana watoto wake Mateo, Thiago na Ciro kwenye macho ya media.

Kwa Georgina yeye ni tofauti, hupendelea zaidi kuonekana kwenye jamii na hivi karibuni alionekana kwenye kipindi kilichorushwa Netflix kiitwacho I Am Georgina ambacho kinaelezea maisha yake binafsi.

Kupitia kipindi anadaiwa kukunja zaidi ya Pauni 9 milioni. Kwenye masuala ya ujasiria mali, Antonella anamiliki kampuni ya mavazi iitwayo Enfans inayopatikana huko Argentina.

Georgina yeye ni balozi wa makampuni mbali mbali ikiwemo Elisabetta Franchi na Amara Lenses ambazo zinampa mpunga wa kutosha ili kutangaza bidhaa zao.

BATA Kwenye sekta hii wote wapo vizuri. Messi na Ronaldo wote wana ndege zao binafsi wanazozitumia kwenye safari mbali mbali pia wanamiliki boti za kifahari.

Antonella na Georgia wamekuwa wakionekana kwenye fukwe mbali mbali na wenza wao wakati wa mapumziko.

Muda mwingi kabla ya ligi kuanza familia hizi mbili utaziona Hispania, Italia au Ugiriki zikila bata huku pembeni kukiwa na maboti yao yenye kila kitu ndani yake.

Cristiano na Georgina pia waliwahi julala kwenye hotel moja hiko Majorca Hispania ambayo kwa usiku mmoja hugharimu Pauni 10,000 ambazo ni zaidi ya milioni 30 za kibongo.

MAGARI Kwanza Ronaldo mwenyewe ana magari uanayokadiriwa kufikia thamani ya Pauni 18 milioni.

Kama ilivyo yeye, mchumba wake Georgia pia anaendesha ndinga za thamani. Mbali ya kuendesha ndinga hizo mara kadhaa amekuwa akimshangaza Ronaldo kwa zawadi za magari mbali mbali.

Mara ya kwanza alimnunulia gari ya Pauni 516,000 aina ya Mercedes G-Class Brabus SUV.

Kisha mwishoni mwa mwaka jana akamnunulia tena ndinga yenye thamani ya Pauni £250,000 aina ya Rolls-Royce Dawn.

Messi, pia ana magari kibao ya kifahari lakini hiyo ni tofauti na mkewe Antonella ambaye hajawahi kuonekana akiendesha magari ya thamani.

Alionekana mara moja tu akiendesha gari ndogo aina ya Mini Cooper inayotumia umeme akipita nayo mitaa ya Paris. Gari hiyo inakadiriwa kuwa inauzwa Pauni 31,000.

WALIVYOKUTANA Georgina alikutana na Cristiano wakati anafanya kazi Jijini Madrid katika duka la Gucci mwaka 2016 wakati huo akiwa anapata mshahara wa Pauni 250 kwa wiki kutokana na kazi hiyo.

pia wakakutana kwenye sherehe za Gucci siku chache baadae. Georgia mwenyewe anasimulia kwamba walipendana mara tu baada ya kuonana kwa mara ya kwanza.

Uhusiano wa ulikuwa wa siri kwa miezi kadhaa lakini ilipojulikana watu wakaanza kujazana kwenye duka alilokuwa anafanya kazi Georgia na wingi wa mashabiki hao ulisababisha Georgia afukuzwe kazi Desemba 2016 ili kuepusha kadhia hiyo kwani mabosi waliona mashabiki hao wanaweza hata kuvunja duka.

Antonella yeye ni mchumba wa muda mrefu wa Messi. Wawili hawa walianza uhusiano tangu mwaka 2007, wote wawili walikukua maeneo ya Santa Fe, Argentina, kavla ya Messi kujiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13, kisha baadae wakaungana tena nchini Hispania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live