Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu haya kuhusu Yanga kabla hajakutana na Kagera

Yanga WA0042 Fahamu haya kuhusu Yanga kabla hajakutana na Kagera

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimeshindwa kupata goli lolote kwenye mchezo mmoja pekee wa ligi kwenye michezo mitano ya karibuni.

Yanga haijafunga goli lolote kwenye michezo 2 pekee ya ligi tangu msimu uanze ambayo iliisha Kwa Sare ya 0-0 dhidi ya Kagera Sugar lakini dhidi ya JKT Tanzania, Michezo yote Yanga walikuwa ugenini.

Yanga imeshinda michezo minne kati ya mitano ya karibuni huku ikiwa haijapoteza mechi yeyote. Yanga wamecheza michezo minne bila kuruhusu nyavu zao kuguswa.

Kagera Sugar imepoteza mchezo mmoja kwenye michezo mitano ya karibuni (1 Kupoteza, 1 kushinda, 3 sare).

Kagera Sugar wamecheza michezo minne bila kuruhusu goli lolote, timu ya mwisho kuwafunga Kagera kwenye ligi kuu ilikuwa ni Namungo kwenye ushindi wa 1-0 mwezi March mwaka huu.

Kagera Sugar haijapoteza mchezo wowote wa ugenini kwenye michezo 3 ya karibuni (Sare 2 na ushindi mara 1).

Head to Head Michezo 3 ya mwisho baina ya timu hizi Yanga ameshinda mara 2 na mchezo 1 pekee ulimalizika Kwa Sare.

Yanga imefunga magoli 6 kwenye michezo 3 ya mwisho, huku Kagera Sugar wakiwa hawajafunga goli lolote.

Kwenye msimamo wa Ligi Yanga anaongoza akiwa amecheza mechi 25 na alama 65, ameshinda mechi 21, kupoteza mbili na sare mbili. Amefunga mabao 56 na kuruhusu mabao 12 na yupo mbioni kuutwaa ubingwa kwa mara ya 30.

kagera yupo nafasi ya 7 akiwa na alama 30 kwenye michezo 25 aliyocheza. Ameshinda mechi 6, kupoteza 7 na sare 12. Amefunga mabao 17 na kufunga 21.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live