Kiungo wa Namungo FC Ibrahim Mkoko ametia chuma tatu (3) pekeyake ‘hat-trick’ dhidi ya KMC FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu na kuisaidia timu yake kuondoka na alama tatu (3) ugenini.
Zipo hat-trick nyingi, kwa hiyo Mkoko amefunga perfect hat-trick ambayo kwa mara ya kwanza imefungwa katika Ligi Kuu Bara kwa msimu huu.
Maana ya perfect hat-trick ni kufunga mabao matatu ndani ya mchezo mmoja kwa kutumia viungo vyote muhimu vya mwili vinavyotumika katika kuchoza soka yaani mkuu wa kulia, mguu wa kushoto na kichwa kwenye mechi moja.
FT | KMC FC 1-3 Namungo FC
⚽ 40' Ibrahim Mkoko (Mguu wa kushoto)
⚽ 57' Ibrahim Mkoko (Kichwa)
⚽ 59' Kelvin Kijiri
⚽ 90+5' Ibrahim Mkoko (Mguu wa Kulia).