Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fagio la kufa mtu kupita Spurs

Hugo Loris Astaafu France 56303804

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Tottenham Hotspur, Hugo Lloris anajiandaa kuongoza kundi kubwa la mastaa wa timu hiyo watakaoonyeshwa mlango wa kutokea kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi wakati kocha mpya Ange Postecoglou akijipanga kupitisha panga ili kubaki na wachache kabla ya kusajili wapya.

Kocha huyo raia wa Australia, Postecoglou, ambaye aliongoza Celtic kushinda mataji matatu ya ndani huko Scotland msimu uliopita, anataka kuanza upya kabisa kwenye kikosi cha Spurs baada ya kushindwa kukamatia tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.

Ripoti zinafichua kwamba kuna wachezaji wengi watafuatana na Lloris kuelekea mlango ulioandikwa ‘exit’ wakiwamo pia Joe Rodon na Sergio Reguilon, ambao walikuwa kwa mkopo Rennes na Atletico Madrid mtawalia, hawatarudi huku wengine ni Davinson Sanchez, Japhet Tanganga, Harry Winks, Giovani Lo Celso na Tanguy Ndombele, Alfie Devine na Ivan Perisic.

Kuna wasiwasi wa kuhusu straika Harry Kane, ambaye anasakwa na timu nyingi ikiwamo Manchester United na Bayern Munich, huenda akauzwa huku Son Heung-min akitarajia kubaki licha ya kutakiwa huko Saudi Arabia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live