Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fagio; Mastaa hawa kutimuliwa Singida FG

Kazadi Fagio; Mastaa hawa kutimuliwa Singida FG

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa Singida Big Stars wameanza harakati kimyakimya za kuangalia majina ya wachezaji wa kuachana nao kutokana na kuonyesha viwango duni, huku mshambuliaji wa kikosi hicho, Francy Kazadi akiwa ni miongoni mwao waliopo hatarini kupigwa panga katika dirisha dogo.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo zimesema, wapo mastaa ambao wanafanyiwa tathimini kuanzia sasa na kama benchi la ufundi halitaridhika na viwango vyao watapewa mkono wa kwaheri dirisha dogo litakapofunguliwa.

“Ni kweli tumeanza kufanya tathimini ya kila mchezaji lakini tunaangazia sana kwa wale wa kigeni kwa sababu ndio ambao tunatumia fedha nyingi kuwalipia, Kazadi ni miongoni mwao ila ni mapema na lolote linawezekana,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Ibrahim Mirambo akizungumzia hilo alisema wao kama viongozi wana mambo mengi ya kufanya hasa kuangalia namna timu hiyo inaleta ushindani hivyo suala la nani ataachwa ni mapema mno kulizungumzia.

“Ndio kwanza tuko Oktoba na dirisha linafunguliwa Desemba sasa ukiangalia kuna muda kama wa miezi miwili imebaki, siwezi kusema moja kwa moja kuhusu hilo kwa sababu litabaki kwenye ripoti ya benchi la ufundi la nani abaki na wa kuachwa,” alisema Mirambo.

Kazadi amekuwa katika kipindi kigumu tangu ajiunge na kikosi hicho dirisha dogo la Januari mwaka huu baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi alipoibuka mfungaji bora kufuatia kufunga jumla ya mabao sita.

Nyota huyo alijiunga akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na klabu ya Al Masry ya nchini Misri huku akiwahi kuzichezea timu mbalimbali kama AS Vita Club, DC Motema Pembe za kwao Congo na Wydad Casablanca na SC Chabab Mohammedia za Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live