Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fadlu: Vilio Simba sasa basi

Gamondi Fadlu Mez Fadlu: Vilio Simba sasa basi

Sat, 24 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amejivunia muunganiko wa timu yake, anatarajia wachezaji wake kauonyesha kiwango bora katika mchezo wa kesho dhidi ya Fountain Gate FC.

Simba wanashuka dimbani kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Fountain Gate FC, utakaochezwa uwanja wa KMC, uliopo Mwenge Dar es Salaam.

Fadlu amesema maandalizi ya mchezo wa kesho yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri ya kuonyesha ushindani mkubwa kwa ajili ya kutafuta matokeo chanya.

Ameeleza kuwa kikosi kinaendelea kupata muunganiko mzuri na timu inatengeneza nafasi kuanzia nyuma katika idara ya ulinzi mpaka ushambuliaji.

“Tungekuwa makini katika mchezo uliopita dhidi ya Tabora United tulikuwa tunaweza kupata ushindi mnono zaidi ya mabao matatu tuliyofungwa.

Kikosi kinazidi kuimarika siku hadi siku, timu ipo kwenye umbo zuri tunatengeneza mashambulizi kuanzia nyuma kwenda mbele na maelewano ni makubwa,” amesema Fadlu.

Nahodha wa Simba, Mohammed Hussein, ‘Zimbwe Jr ‘, amesema wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo ya kocha ili kuisaidia timu matokeo chanya.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, Fountain Gate FC, wana timu imara lakini tumejipanga tayari kuwakabili na tutafuata maelekezo kusaidia timu kupata matokeo chanya,” Zimbwe Jr.

Naye Kocha wa Fountain Gate FC, Mohammed Muyya amesema wanaiheshimu Simba timu kubwa wamewekeza na wao ni wakubwa na anatarajia kufanya vizuri.

“Haitakuwa mechi rahisi, vijana wangu wanahitaji kufika mbali kuonyesha mchezo mzuri kesho dhidi ya Simba, tutaonyesha mchezo mzuri na kuwapa ushindani,” amesema Muyya.

Kuhusu kucheza dhidi ya Simba, Kocha huyo amesema sio mara ya kwanza kuongoza benchi la ufundi dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi alifanya hivyo akiwa Dodoma jiji FC.

“Tuna waheshimu Simba tunawaheshimu hatuwaogopi, tumewaona wapinzani wetu walipocheza mechi ya kwanza wana kocha mpya na wachezaji wapya, hakuna tofauti hata sisi tupo kwenye kutengeneza timu,” amesema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live