Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fadlu, Kijili wakoleza moto Simba

Badlu David Simba Fadlu Davis

Sat, 13 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba ikimtambulisha beki wa kulia, Kelvin Kijili, mratibu wa timu hiyo, Abbas Ally amesema wachezaji wameanza kumpa ushirikiano mzuri kocha, Fadlu Davis baada ya kuwapa mikakati yake,

Amesema umekuwa mwanzo mzuri katika maandalizi ya msimu wa 2024/25 na wachezaji wameingia kwenye mfumo wa kocha huyo anahitaji anahitaji kitu gani kutoka kwao kufikia malengo hayo.

Simba ipo katika jiji la Ismailia nchini Misri kuendelea na maandalizi ya msimu ujao na mechi zisizopungua nne au tano huku mechi ya kwanza wakitarajia kucheza Julai 15 au 16, mwaka huu nchini humo.

“Baada ya Kocha Fadlu kutua kambini, amezungumza na wachezaji akiwaeleza falsafa yake , wameanza kuelewana na matarajio makubwa ya kufanya vizuri msimu ujao, mechi za kirafiki zitakuwepo tutacheza kuanzia wiki ijayo,” amesema Abbas.

Simba imemtambulisha, beki wa kulia Kelvin Kijili akitokea Singida Fountain Gate kwa mkataba wa miaka miwili.

Beki huyo anaungana na Isarel Mwenda na Shomari Kapombe ambaye amejihakikishia namba ndani ya kikosi cha Simba kwa kila kocha nayekabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi cha timu hiyo.

Wakati huo huo, Meneja wa idara ya habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amemmwagia sifa Kijili na kusema kuwa ni kijana mwenye kipaji na kasi amekuwa akitumika kuanzisha mashambulizi kutokea upande wa kulia.

“Alipokuwa Singida Fountain Gate msimu uliopita alichangia kupatikana kwa mabao manne, amekuja Simba kuongeza kitu kikubwa kwenye kikosi chetu kwa sababu na umri alionao tunaamini ataendelea kuwa msaada kwa timu,” amesema Ahmed.

Amesema usajili walioufanya kuelekea msimu mpya wa mashindano wamezingatia kigezo cha umri kwa kuwa malengo yao ni kujenga timu imara ya muda mrefu.

Beki huyo amejiunga na wachezaji wenzake kambini nchini Misri katika jiji la Ismailia kuendelea na maandaliz ya msimu mpya wa mashindano ya 2022/25

Chanzo: www.tanzaniaweb.live