Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fadlu: Dabi ya kesho itakuwa na mabao mengi

Gamondi, Fadlu Fadlu: Dabi ya kesho itakuwa na mabao mengi

Wed, 7 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amewataka mashabiki na wananchama wa timu hiyo kutokuwa na presha na kusahau kuhusu kipigo cha bao 5-1 walichokipokea msimu uliopita kutoka kwa watani zao, Yanga SC.

Fadlu ambaye amejiunga na Simba msimu huu amesema kuwa mchezo wa kesho wa Ngao ya jamii dhidi ya Yanga watauendea kama michezo mingine yoyote na kulingana na mipango yake pamoja na uwezo wa wachezaji wake, anaamini watapata ushindi.

"Yanga sio tu kwamba wana wachezaji wazuri, bali wana kocha mzuri, benchi bora la ufundi, tumeona msimu uliopita walikuwa na mbinu tofauti tofauti hasa kwenye kujilinda kulingana na mpinzani wanaokutana naye, tunaamini tutausoma mpango wao na kuuelewa jinsi wanavyojipanga kwenye kulinda.

"Na sisi tutaleta mpango wetu na kuangalia mapungufu yao yalipo. Kutokana na uwezo wa wachezaji wetu ambao wana vipaji vikubwa vya aina tofauti kwenye kukaba na kushambulia na wenye mbinu nyingi, lakini lazima ku-balance timu kutokana na uwezo wa mpinzani wetu kushambulia.

"Hatutakaa nyuma muda wote kuzuia ama kushambulia muda wote, tutatengeneza mpango ambao utatupa matokeo mazuri kwenye mchezo huo. Itakuwa mechi ya kushambuliana kwa zamu, kama tuki-balance vizuri timu yetu, ninaamini tutapata nafasi ya kufunga mabao na hii mechi ninaamini itakuwa na mabao mengi," amesema Fadlu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: