Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fabregas: Man U? Kuna kitu hakipo sawa

Screenshot 20231113 163724 Kocha Cesc Fabregas

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Cesc Fabregas amezungumzia kushuka viwango vya mastaa Jadon Sancho, Casemiro na Sofyan Amrabat kunathibitisha ukweli kwamba kuna kitu hakipo sawa Manchester United.

Man United imekuwa na msimu wa hovyo, ikimaliza nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu England na ilitupwa nje ya Kombe la Ligi kwenye raundi ya nne huku ikikomea hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, tena kwa kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi.

Msimu huo umeshuhudia pia kushuka viwango kwa mastaa kadhaa, huku Sancho akitibuana na kocha Erik ten Hag kabla ya kurudi kwa mkopo Borussia Dortmund, ambako amekuwa moto.

Casemiro naye kiwango chake kilishuka kwa kasi, sawa na Amrabat ambaye alikuwa moto kwenye Kombe la Dunia 2022 kabla ya kwenda kuwa wa kawaida sana huko Man United.

Na sasa, Fabregas anabainisha kwamba kushuka viwango kwa wachezaji hao watatu si jambo linaloweza kutokea tu kwa bahati mbaya.

“Manchester United inaweza kurudi kwenye ubora kwa sababu ni timu kubwa, lakini mtazame Jadon Sancho. Hakuwa anafanya vizuri Man United, alipokwenda Dortmund amerudi kuwa yule mchezaji wa zamani,” alisema Fabregas.

“Ona yule kiungo aliyetamba na Morocco kwenye Kombe la Dunia (Amrabat), alikuwa bora sana. Amekwenda Man United na hapo amekuwa si yule tena. Casemiro alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Real Madrid. Alikuwa kiungo bora kabisa mkabaji wakati anatua Man United, lakini kwa sasa anaonekana kuwa mchezaji tofauti kabisa. Nadhani kuna kitu hakiendi sawa pale. Sio kitu cha bahati mbaya, wachezaji watatu wa viwango vya juu wote kushuka viwango ghafla.”

Licha ya kuwa na msimu wa hovyo kwenye ligi, Man United imeshinda ubingwa wa Kombe la FA baada ya kuwachapa mahasimu wake Manchester City, huku kocha Ten Hag akidai kwamba kufeli kwa timu kumesababishwa na majeruhi wengi kikosini.

Chanzo: Mwanaspoti