Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FLASHBACK: Tshabalala, Staa wa Soka anaemilikiwa na Baba "Watatu"

Siphiwe Tshabalala Tshabalala Staa wa Soka asiemtambua baba yake

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondeni kabisa Kwa Madiba katika mji mmoja wa Soweto mitaa iliyojaa wahuni na vichaa wengi, mitaa ambayo mtu kupigwa risasi sio mada, Mada ni nani anafuatia kupigwa risasi jioni.

Ni hapo ambapo Kwaito imezaliwa ila nyimbo za vurugu na maandamano ndio zinaimbwa sana.Miezi tisa inatimia Black beauty mmoja Hafidele Rebecca analia kwa uchungu juu ya kitanda, siku ambayo Lawrence Siphiwe Tshabalala anazaliwa. Ilikuwa ni tarehe 25 mwezi Septemba mwaka1984 Soweto wanampokea huyu mchawi.

Siphiwe Tshabalala left footer mmoja anakuja kuitakasa jezi ya Bafana Bafana kwa baraka za "Father of Soweto" James Mpanza na uchawi wa miguu yake kwenye dimba la Soccer City.

Najua mitaa na wana wa Banda Umiza nimewakumbusha Kombe la Dunia 2010 pale Bondeni. Yes, wote hatujasahau kitu alichokifanya mbele ya viburi wa kusini mwa Amerika.

Siphiwe Tshabalala, mguu wa mpira pembeni ya mafundi kama Teko Modise na Steven Pieneer angeweza kutokea Winga ya kushoto kisha akafunga kama namba tisa, "One of the Icon Cellebration to remember" anafunga goli la kwanza la michuano ya kombe la dunia 2010, kisha anatupa ofa ya staili tamu ya kushangilia pembeni ya Kibendera, Afrika inafurahi ni Soweto to the World. South Africa 1- Mexico 0 dakika ya 54 hapo nipo juu ya dirisha la watu napambana na mimi nimuone huyu mtu.

Mpaka leo haijulikani Baba yake halisi ni nani, zaidi ya wanaume watatu wanadai Siphiwe ni damu yao. Kipindi anazaliwa mama yake alikuwa anatoka na mtu mmoja anaitwa Isaac Tshabalala ndie aliyempa jina la Siphiwe.

Mnisamehe ndugu zangu, siku moja nitakuja na stori za huyu Mwamba ndani ya uzi wa Kaizer Chiefs mpaka Amazulu kuna simulizi tamu sana zimeandikwa kuhusu yeye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live