Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yawachinjilia mbali Benin, Afrika ya Kusini

 121560281 Sa Ghana Getty 1235088159 Kikosi cha Timu ya Taifa ya Afrika ya Kusini

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) wametupilia mbali malalamiko ya Benin ya kuomba DR Congo ipokwe alama 3 kwa kufanya mabadiliko ya wachezaji 5 kwa zaidi ya awamu 3.

Sheria za FIFA zinaruhusu mabadiliko ya wachezaji watano lakini kwa awamu ama mikupuo mitatu tu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, DR Congo haiadhibiwi kwa sababu kosa ni la waamuzi wa mechi katika mchezo huo wa kundi J.

Katika sakata jingine, malalamiko ya Afrika Kusini dhidi ya Ghana wakiomba mechi yao ya kuwania kufuzu hatua ya mchujo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia kwa upande wa Afrika pia yametupiliwa mbali kwa vile yaliwasilishwa nje ya muda stahiki.

Timu ya taifa ya Afrika Kusini “Bafana Bafana” ilitoa malalamiko kwa Shirikisho la Kandanda Duniani Fifa kuwa ushindi ambao Ghana waliupata wa goli 1-0 mwezi Novemba haukuwa sahihi baada ya goli pekee kufungwa kwa njia ua penati ambayo wanadhani haikuwa halali.

Kutupilia mbali madai hayo, inamaanisha kuwa Ghana itakuwa moja ya timu 10 ambazo mwezi Januari 2022 zitakuwa kwenye droo ya kupangiwa mshindani kabla ya kupatikana kwa timu tano pekee zitakazoliwakilisha bara la Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live