Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yashinikizwa kuiondoa Iran Kombe la Dunia

Iran Team FIFA yashinikizwa kuiondoa Iran Kombe la Dunia

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Duniani FIFA linakumbana na shinikizo la kuiondoa timu ya Taifa Iran kwenye michuano ya kombe la Dunia 2022.

Rais wa FIFA Gianni Infantino amepokea barua kutoka kwa OPEN STADIUMS ikieleza kwa kina jinsi wanawake wanavyotendewa na mamlaka za Iran, ikiwa ni pamoja na ukatili dhidi ya wanawake na kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa kujaribu kuhudhuria michezo nchini humo.

OPEN STADIUMS ni kundi la wanaharakati Wanawake wanaotetea na kupinga sheria ya Iran inayozuia Wanawake kuhudhuria viwanjani kutazama michezo.

Katika barua hiyo Open Stadiums wamehoji “Kwa nini FIFA imeipa taifa la Iran na wawakilishi wake hatua ya kimataifa, huku ikiwa imeshindwa kuheshimu haki za msingi za binadamu kwa kuwatesa na kuwaua watu wake wenyewe? Vifungu vya sheria vya FIFA viko wapi katika suala hili?

“Tunaiomba FIFA, kwa kuzingatia vifungu vya 3 na 4 vya sheria zake, kuiondoa mara moja Iran kwenye Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar.”

Kufuatia sakata hilo mashabiki katika mitandao ya kijamii wameunga mkono hatua hiyo huku baadhi wakiitaka Ukraine ipewe nafasi ya Iran kwenye michuano ya kombe la Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live