Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yamfungia Nsue na timu yake ya Taifa

Emilio Nsue C Emilio Nsuè

Sat, 25 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya nidhamu chini ya FIFA imeifungia nchi ya Equatorial Guinéa sambamba na mshambuliaji Emilio Nsuè López (34) kutokana na walakini uliojitokeza kwa mshambuliaji huyo mzaliwa wa Hispania.

FIFA imejiridhisha kuwa Nsue hakukidhi vigezo vya kuitumikia Equatorial Guinea kwenye mashindano yoyote yanayohusisha mpira wa miguu.

Mfungaji bora huyo wa AFCON 2023 amefungiwa kutogusa mpira wa miguu kwa kipindi cha miezi 6.

FIFA pia wamezipa ushindi wa goli 3-0 timu za taifa za Namibia na Liberia dhidi ya Equatorial Guinéa kwenye kampeni ya kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026 kufuatia walakini huo.

Chama cha soka nchini Equatorial Guinea pia kimetozwa faini ya kiasi ya Dolla USD $164,092.95. Takribani Tsh 350 millioni za Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live