Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yakwaa kisiki na mpango wake wa mabadiliko

FIFA Logo 1050x700 FiFA yapingwa mabadiliko Kombe la Dunia

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vilabu vya Premier League Vinapinga kwa kauli moja mipango ya FIFA ya kupanga upya kalenda ya mechi kuanzia 2024, ambayo itajumuisha Kombe la Dunia linalofanyika kila baada ya miaka miwili.

Baraza linaloongoza linafanya upembuzi yakinifu wa kufanyika kwa Kombe la Dunia la wanaume na wanawake kila baada ya miaka miwili kuanzia 2028 kama sehemu ya upangaji upya wa kalenda ya soka.

Mipango hiyo ni chimbuko la kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger, ambaye sasa ni mkuu wa maendeleo ya soka duniani FIFA.

Chini ya mapendekezo hayo, mechi zote za kufuzu za kimataifa pia zingechezwa katika kundi moja wakati wa Oktoba.

Katika taarifa kufuatia mkutano wa hivi karibuni wa wanahisa wa vilabu, Ligi Kuu ya Uingereza ilisema: “Vilabu vyote 20 vya Ligi Kuu vimejadili mchakato wa mapinduzi ya Kalenda ya Mechi za Kimataifa ya 2024 na wanapinga kwa kauli moja pendekezo la FIFA la Kombe la Dunia la wanaume kufanyika kila baada ya miaka miwili.

“Vilabu viliibua wasiwasi kuhusu athari mbaya ambazo mapendekezo ya sasa ya FIFA yangekuwa nayo kwa ustawi wa wachezaji, uzoefu wa mashabiki, maandalizi ya kabla ya msimu na ubora wa mashindano.”

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA na ligi zingine kuu za Ulaya pia zinapinga mipango hiyo, ambayo inatazamiwa kupigiwa kura na nchi 211 zinazotambuliwa na FIFA.

Mtendaji mkuu wa EPL Richard Masters alisema ligi kuu ya Uingereza “iko wazi kwa mabadiliko na mawazo mapya” lakini ni yale tu ambayo yangeboresha mchezo.

Masters alisema: “Premier League imejitolea kuzuia mabadiliko yoyote makubwa kwenye Kalenda ya Mechi ya Kimataifa ya FIFA ya baada ya 2024 ambayo yataathiri vibaya ustawi wa wachezaji na kutishia ushindani, kalenda, miundo na mila ya soka ya ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live