Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mighh (FIFA) limeiondolea Simba SC, adhabu ya kufungiwa kusajili baada ya kuilipa Klabu ya Teungueth ya Senegal.
Awali, FIFA iliifungia klabu hiyo ya Ligi Kuu ya NBV baada ya kushindwa kuilipa Teungueth kutokana na mauzo ya mchezaji Pape Ousmane Sakho.
Klabu hiyo ilifungua kesi FIFA dhidi ya Simba ikidai sehemu ya malipo kutokana na mauzp ya Sakho. Simba ilishindwa kesi hiyo na kutakiwa kuilipa klabu hiyo ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini haikutekeleza na kusababisha ifungiwe.
Baada ya kukamilisha malipo hayo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania nalo limeifungulia Simba kyfanya usajili wa ndani wa wachezaji hiyo ni kwa mujibu wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo.