Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yaikalia kooni Wydad mabilioni ya Msuva

Msuva Ml.jpeg Simon Msuva

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeiagiza klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kumlipa mchezaji Simon Msuva zaidi ya dola za kimarekani 700,000 (zaidi ya bilioni 1.6 za Kitanzania) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya Wydad.

Wydad, aliagizwa kumlipa pesa hizo Msuva, kabla ya 2022 kumalizika ila Msuva amethibitisha kutolipwa pesa hizo mpaka sasa akiwa yuko huko Saudi Arabia,

Ikiwa CAF watafuata kanuni klabu ya Wydad, itafungiwa kucheza michuano ya CAF kulipa faini pamoja na kupokonywa point au kushushwa katika ligi kuu yao ya Morocco.

Msuva ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne alilazimika kuusitisha mkataba wake Disemba mwaka 2021 kutokana na kuidai klabu hiyo malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili (signing fee).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live