Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yaifungia Tabora United kusajili wachezaji

Tabora United Wafungiwa FIFA.jpeg FIFA yaifungia Tabora United kusajili wachezaji

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa taarifa ya kufungiwa kusajili wachezaji kwa klabu ya Tabora United (Kitayosce) inayoshiriki Ligi Kuu baada ya Evariste Mutambay Kayembe kuhinda kesi ya mdai dhidi ya timu hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa uamuzi huo ulikuja baada mchezaji huyo raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) alifungua kesi FIFA akidai malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mishahara

"Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu FIFA baada ya mchezaji Evarist Mutambay Kayembe kushinda kesi ya madai dhidi ya kabla hiyo. Mchezaji huyo raia wa DR Congo alifungua kesi FIFA akidai malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mshahara”

"Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini haikutekeleza hukumu hiyo” imesema taarifa hiyo

Chanzo: Mwanaspoti