Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yaifungia Singida FG kusajili

Rodrigo Figueiredo Carvalho Rodrigo Figueiredo Carvalho.

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Ligi Kuu ya NBC ya Singida Fountain Gate FC imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Rodrigo Figueiredo Carvalho.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la kimaitafa la mpira wa Miguu (FIFA) baada ya Carvalho kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Mchezaji huyo raia wa Brazil alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara.

Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimaitafa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.

TFF inazitaka klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live