Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yaifungia Singida FC kufanya usajili

Kikosi Cha Singida Big Stars 1 1080x640 FIFA yaifungia Singida FC kufanya usajili

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Ligi Kuu ya NBC ya Singida Fountain Gate FC, imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wao Shafik Batambuze.

Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Mchezaji huyo raia wa Uganda alifungua kesi FIFA akidai malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mishahara.

Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolelewa lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

TFF nao wameifungia Singida kufanya uhamisho wa ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live