Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yaifungia Biashara United

Biashara United Championship FIFA yaifungia Biashara United

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limeifungia Klabu ya Ligi ya Championship ya NBC, Biashara United kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Tayo Odongo.

FIFA imetoa uamuzi huo baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Mchezaji huyo raia wa Uganda alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara.

Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Hata hivyo wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.

TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live