Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yafafanua AC za uwanjani kuzimwa wakati wa mechi ya England vs USA

Air Conditions FIFA yafafanua AC za uwanjani kuzimwa wakati wa mechi ya England vs USA

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FIFA inadai kuwa hakukuwa na matatizo ya kiyoyozi kwenye Uwanja wa Al Bayt wakati wa mchezo wa England na Marekani baada ya wachezaji kadhaa wa kocha Gareth Southgate kulalamika kuwa kulikuwa na joto sana.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Mail limeandika kuwa udhibiti wa hali ya hewa katika Uwanja wa Al Bayt ulifanyika saa moja kabla ya kuanza kwa ombi la meneja wa uendeshaji wa FIFA.

Ingawa hakuna pendekezo kwamba malalamiko rasmi yanapaswa kutolewa, baadhi ya kikosi cha Southgate kilitoa maoni kuhusu jinsi kilivyohisi joto kufuatia mchezo huo. Walionekana wanyonge wakati fulani kwenye uwanja huo ambao uliwahi kukumbwa na matatizo, huku mashabiki na wachezaji wakilalamika kuwa walikuwa na baridi sana.

Masharti yanazingatiwa kwa msingi wa kila mechi ikibidi, halijoto huwa nyuzi 24 kwa kila mechi na mchezo wa England haukuwa tofauti. Kwa baadhi ya michezo ya baadaye, kiyoyozi huzimwa saa moja kabla ya kuanza na ndivyo ilivyokuwa Ijumaa usiku.

FIFA haikuruhusu waandishi wa habari kusoma kifaa maalum cha kupima joto ‘wet bulb’, unaochanganya joto, unyevunyevu na mambo mengine, ikiwa ni pamoja na usawa wa jua na kasi ya upepo na ambayo ilitumika Brazil kuamua mapumziko ya vinywaji. Halijoto pekee sio kiashirio sahihi.

Inaeleweka kuwa hali hiyo inarekebishwa kwa msingi wa kesi baada ya nyingine, na mechi za saa 1:00 na 16:00 kwa saa za ndani ziko katika hatari kubwa ya kuongezeka kwa joto.

 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live