Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA waiondolea adhabu Yanga

Bigirimana Hersi Ms FIFA waiondolea adhabu Yanga

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeiondolea Yanga adhabu ya kufungiwa kusajli Wachezaji baada ya kukamilisha malipo ya aliyekuwa Mchezaji wake Gael Bigirimana.

Awali mchezaji huyo alifungua kesi FIFA dhidi ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya NBC kwa kushindwa kumlipa baada ya kumvunjia mkataba.

Bigirimana alishinda kesi hiyo, na Yanga ilitakiwa kumlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo wa FIFA ulipotolewa lakini haikutekeleza na kusababisha ifungiwe kusajili.

Baada ya kukamilisha malipo hayo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungulia Yanga kufanya uhamisho wa ndani wa Wachezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live