Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limeweka utaratibu maalum wa kuvilipa vilabu za Ulaya kutokana na wachezaji wake kutumika kwenye fainali za kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Kutokana na hiyo, Vilabu vya Man City, Man United na Chelsea pamoja na Vilabu vya Hispania vitaingiza pesa nyingi zaidi huku kiasi cha dola 10,000 italipwa kwa Mchezaji mmoja kwa siku.
Aidha, mfumo huo maalum iitwao "Club Benefit Fund" thamani yake itaongezeka kadri Wachezaji wanavyoisogelea fainali ndipo wanaongeza nafasi ya kutengeneza pesa zaidi kwa klabu zao.
World Cup ya 2018, Man City waliingiza kiasi cha dola million tano huku mwaka huu Chelsea ndio watakaongiza zaidi kutokana na kutarajiwa kuwa na wachezaji zaidi ya 20.