Thu, 5 Oct 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Imeripotiwa kuwa shirikisho la soka Duniani FIFA lina mpango wa kuifutia adhabu Urusi ambayo walipewa mara baada ya kutokea vita kati ya taifa hilo dhidi ya Ukraine.
FIFA waliiondosha Urusi kushiriki mashindano yote ambayo yapo chini yake kufuatia sakata la vita ambayo bado inaendelea.
Inaelezwa kuwa Urusi wataruhusiwa kushiriki michuano ya kombe la dunia chini ya umri wa miaka 17 itakayoanza kutimua vumbi Novemba 10, 2023 huko Indonesia.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live