Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeripotiwa kuwa kwenye mpango wa kuleta sheria mpya ‘Game Clock’ kwenye mpira wa miguu, ambapo saa ya mwamuzi itakuwa ikisimama kila muda ambao mpira utakuwa haupo mchezoni (Out of play) hii ni kwa lengo la kukomesha vitendo vya kupoteza muda.
Wazo hili limeletwa na Rais wa FIFA Gianni Infantino kufuatia uzoefu uliopatikana kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 ambapo ilishuhudiwa dakika nyingi zaidi za nyongeza kwenye historia ya mpira wa miguu.
Hoja hii tayari ipo mezani na itaanza kujadiliwa kwenye Kikao cha vyama vya soka kitakachofanyika Jijini London wikendi ijayo.