Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA kuifungia Yanga kufanya usajili, kisa ni hiki..

Luc Aymel Aliekuwa Kocha wa Yanga, Luc Eymael

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Duniani FIFA, limeiamuru Klabu ya Yanga kumlipa aliekuwa Kocha wake raia wa Ubelgiji, Luc Eymael kiasi cha Dola za Kimarekani 152,000 (Sh 354 milioni) ndani ya siku 45, baada ya kocha Luc Eymael kushinda kesi dhidi yao.

FIFA itaiadhhibu klabu ya Yanga kutosajili ndani ya vipindi vitatu mfululizo, ikiwa watashindwa kulipa fedha hizo.

Kocha Luc Eymael alitimuliwa na Yanga Julai 27, 2020 akapeleka shauri hilo FIFA baada ya kutoridhika na kuondolewa kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live