Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA: Mchezo wa Brazil vs Argentina kurudiwa tena

Brazil Vs Argentina Afisa wa afya akimzuia mchezaji wa Argentina asicheze kwa kuvunja sheria za karantini

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limetumbilia mbali rufani ya Brazil na Argentina ya kutotaka kurudia kucheza mchezo wa kufuzu kombe la dunia baada ya bodi ya inayohusika kuamua kuwa mchezo huo urudiwe tena.

Mchezo huo ambao ulisimama dakika chache baada ya kuanza pale moja ya afisa wa afya wa Brazil kuingia uwanjani na kumzuia moja ya mchezaji wa Argentina anayechezea ligi kuu ya Uingereza kutokucheza na kudai kuwa amevunja kanuni za Uviko-19 ya kutojitenga.

Timu zote zimefuzu kushiriki kombe la dunia nchini Qatar mwaka huu, huku Brazil akiongoza kundi na Argentina akifuata na kushika bafasi ya pili. Lakini shirikisho mpira duniani FIFA mwezi February waliamuru mchezo urudiwe tena.

“Baada ya kuchambua malalamiko ya pande zote na kufuatilia jambo lilitoketa kwenye kesi hii, kamati ya rufani imethibitisha kwamba mchezo utarudiwa,” waraka wa FIFA ulisema.

FIFA awali waltoza faini ya $50,322 kwa vyama vyote viwili vya mpira vya Brazili na Argentina kwa sababu ya kuarishwa kwa mchezo huo. Pia waliwapiga faini nyingine ya kutosimamia vizuri swala la usalama kiasi cha 250,000 Swiss francs ambacho kimepinguzwa na kamati ya rufani hadi 100,000 Swiss francs leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live