Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA Kuchangia Dola Million moja Nchini Ukraine

FIFAAAA FIFA Kuchangia Dola milioni moja Ukraine

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la mpira duniani FIFA limechangia kiasi cha $1million kwa ajiri ya misaada ya kibinadamu nchini Ukraine pia limesafirisha vifaa vya huduma ya kwanza kwa shirikisho la mpira wa miguu nchini Ukraine (AUF) ili kutoa msaada wa kimatibabu.

Mashirikisho mbalimbali ya mpira wa miguu pia yameichangia Ukraine, kwa wiki kadhaa zilizopita tokea nchi hiyo ivamiwe kijeshi na taifa ka Urusi February 24. Ukiacha FIFA, pia UEFA nao walichangia €1million huku EPL wakichangia £1million ili kusaidia watoto wa nchini Ukraine.

Mchango wa FIFA umekuja baada ya mabadiliko ya wiki iliyopita ya kuwasaidia wachezaji wanaocheza ligi kuu ya Ukraine, ambapo klabu za nje zinaweza kuwasajili wachezaji wanaotoka kwenye ligi kuu ya Ukraine nje ya darisha la usajiri wa kawaida, ili kuruhusu wachezaji hao kuendelea kucheza mpira.

Rais wa FIFA Gianni Infantino akitangaza msaada huo alisema, “kwa sura ya huu mzozo, tunataka tufanye kwa sehenu yetu na kusaidia watu wa Ukraine ambao wanakimbia vita.

“FIFA watasimama imara kutoa usaidizi utakaohitajika kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na jumuiya ya mpira wa miguu kwenye ukanda wa Ukraine.”

FIFA waliiondoa nchi ya Urusi kushiriki mashindano yoyote ambayo yanaandaliwa na shirikisho hilo mwezi February, pia rufaa ya Urusi kupinga maamuzi ya kuondolewa kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia, yalitupikiwa mbali na mahakama ya kimichezo (CAS) wiki iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live