Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FGA Talents yarudi upya ikiisaka Ligi Kuu

FGA Talentsssss FGA Talents yarudi upya ikiisaka Ligi Kuu

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya FGA Talents inaendelea na mchakato wa kubadili jina, huku uongozi wa timu hiyo umesema mkakati wao ni kuitafuta Ligi Kuu msimu ujao na kuthibitisha makazi yao rasmi kuwa mjini Songea.

FGA Talent ilikuwa na makazi yake jijini Dodoma, ambapo mwishoni mwa msimu uliomalizika hivi karibuni wa Championship ilicheza mechi mbili katika uwanja wa Majimaji.

Meneja wa timu hiyo, Shaibu Shaban alisema kwa sasa uongozi unaendelea na mchakato wa kubadili jina baada ya kukamilisha taratibu za manunuzi na makazi yao msimu ujao itakuwa Ruvuma.

Alisema wanaendelea kusuka upya timu hiyo kuanzia benchi la ufundi na wachezaji, ambapo wanatarajia msimu ujao wapande Ligi Kuu kutokana na maandalizi na mipango waliyonayo.

“Rasmi timu itakuwa hapa Songea na jina litabadilika, tutakuwa na mabadiliko makubwa kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji, kwa sababu lengo ni kucheza Ligi Kuuâ€

Meneja huyo aliongeza kuwa hadi sasa bado hawajaanza usajili wala kambi kwakuwa wanaenda kuanza mipango mipya hawajaamua wapi waweke timu kwa ajili ya msimu ujao.

“Kuhusu wapi tutaweka kambi kwa maandalizi, au usajili bado tunaweka mipango sawa, hadi mwishoni mwa mwezi huu tutakuwa tumejipata na kuweka wazi†alisema kiongozi huyo.

Kupatikana kwa timu hiyo na Tunduru Korosho ya First League kunaongeza mzuka kwa mashabiki mkoani humo, ambapo tangu Majimaji ipoteane walikuwa na kiu ya kuona burudani.

Chanzo: Mwanaspoti