Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FC Barcelona yashusha presha UEFA

Fc Barcelona Unveil New Signing Robert Lewandowski Scaled 1 1024x683 FC Barcelona yashusha presha UEFA

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona, imeshusha pumzi baada ya kuwa na uwezekano wa kuwatumia wachezaji wake, Pedri, Raphinha na Robert Lewandowski katika mchezo wa EI Clasico, Oktoba 28, mwaka huu.

Wachezaji hao ambao ni majeruhi, kwa sasa wanaendelea vizuri huku timu hiyo ikiwa na mechi mbili kabla ya kukutana na Real Madrid kwenye El Clasico.

Pedri yupo kwenye hatua za mwisho kurejea uwanjani, ambapo juma lijalo anatarajiwa kuungana na wenzake mazoezini, ambapo anaweza kutumika kwa muda mchache mechi mbili zijazo dhidi ya Athletic Club au Shakhtar kabla ya kuvaana na Real Madrid.

Kwa upande wa Raphinha, ana nafasi kubwa ya kucheza dhidi ya Real Madrid kutokana na kuwa na muendelezo mzuri, akitarajiwa kucheza dhidi ya Shakhtar Donetsk katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lewandowski naye siku chache zijazo, anatarajiwa kuanza mazoezi ya kuuchezea mpira kujiandaa na El Clasico.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live