Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FA yawakingia kifua waraibu wa kubet

Nicolo Zaniolo Mm FA yawakingia kifua waraibu wa kubet

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Italia limesema linaendelea kuwaunga mkono wachezaji Sandro Tonali (Newcastle United) na mshambuliaji wa Aston Villa, Nicolo Zaniolo wote raia wa Italia huku wawili hao wakidaiwa kuwa na uraibu wa kamari (kubeti).

Rais wa FA, Gabriele Gravina amesema : “Kama binadamu ninawahurumia wachezaji hao wawili, ni kama watoto kwangu. Hatupaswi kuwashutumu vijana hawa.

“Uraibu wa kucheza kamari si tatizo la soka, ni janga la kijamii. Nakuhakikishia kuwa yeyote anayeomba msaada tutamsaidia.”

"Yeyote aliyefanya makosa ataadhibiwa na kusaidiwa katika mchakato wa kuachana na kamari. Tunahitaji kuwaweka watu hawa kwenye njia ya kupona.

“Inabidi tuhakikishe watoto hawa wanaweza kurudi katika hali ya kawaida. Hatutawaacha kamwe."

Sandro Tonali na Nicolò Zaniolo wanakabiliwa na kashfa ya kamari lakini kesi zao zipo tofauti sana, Tonali anakabiliwa na kashfa ya kubetia mechi za mpira wa miguu. Ikumbukwe, wanasoka hawaruhusiwi kubashiri kwenye mchezo wa soka.

Kwa upande wake Zaniolo anadaiwa kukutwa na hatia ya kutumia majukwaa haramu ya kubeti mtandaoni lakini hakubetia mechi za mpira wa miguu.

Mawakili wa Zaniolo wanadai hakucheza kamari kwenye michezo ya soka bali alibeti kwenye ‘poker’ na ‘blackjack’, bila kujua kwamba kampuni ya kubeti aliyotumia haina leseni.

Kubeti sio kosa la jinai nchini Italia, bali inakuwa kosa ikiwa wanaoweka dau watatumia makampuni/majukwaa ya kubeti yasiyo na leseni na wasioidhinishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live