Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FA yampiga 'stop' Ronaldo

Cr7 Pic Cristiano Ronaldo

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Cristiano Ronaldo alifungiwa kucheza mechi mbili na Chama cha soka FA kabla ya kutimka Ligi Kuu England baada ya kuvunjiwa mkataba na Manchester United mwaka jana.

Kwahiyo Ronaldo atakosa mchezo mwingine wa ligi unaofuata akiwa na klabu ya Al Nassr kutokana na adhabu hiyo anayokabiliana nayo. Hadi tunaingia mtamboni Ronaldo hakucheza mechi yake ya kwanza baada ya utambulisho.

Ronaldo alilimwa faini na FA Novemba mwaka jana baada ya kuipigiza chini simu ya shabiki wa Everton wakati anaingia vyumba vya kubadilishia nguo. Tukio hilo limetokea tangu Aprili mwaka jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, Man United ikipokea kichapo cha bao 1-0.

Licha ya Ronaldo kusaini mkataba mnono Al Nassr ambao uligharimu kitita cha Pauni 173 milioni, Mreno huyo aliwambiwa na FA hataruhusiwa kucheza hadi adhabu hiyo itakapokamilika.

Ronaldo alitambulishwa rasmi na klabu ya Al Nassr mbele ya umati wa mashabiki katika uwanja wa Mrsool Park, unaomilikiwa na klabu hiyo uliyopo ndani ya jiji la Riyadh, Saudi Arabia ambao unaingiza mashabiki 25,000.

Ronaldo aliwasili Saudi Arabia pamoja na familia yake akiambatana na watu wa mambo ya kiufundi na waandishi wa habari.

Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa duniani kukipiga kwenye klabu hiyo kwenye historia ya maisha yake ya soka. Wakati huo huo waziri wa michezo wa Saudi Arabia, Abdulaziz bin Turki Al-Feisal ameahidi atazisapoti klabu zote nchini humo endapo madili makubwa kama hayo yakijitokeza.

Chanzo: Mwanaspoti