Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FA yachunguza Shabiki aliemshambulia golikipa wa Arsenal

Ramsdale = Fans FA yachunguza Shabiki aliemshambulia golikipa wa Arsenal

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki wa Tottenham, Joseph Watt, 35, ameshtakiwa kwa kosa la kumpiga teke kipa wa Arsenal baada ya mechi ya Ligi Kuu England, timu hizo zilipocheza wikiendi iliyopoita.

Shabiki huyo alitinga mahakama ya Hughbury Magistrates kwaajili ya kusisiliza mashtaka baada kukamatwa na polisi juzi. Tottenham ilishirikiana na polisi kwenye uchunguzi wa tukio uliyofanyika katika kutoka kituo cha polisi Metropolitan baada ya shabiki huyo kutambulika.

Baada ya mchezo huo Tottenham ililaani vitendo hivyo na watashirikiana bega kwa bega na polisi hadi uchunguzi utakapokamilika.

Chama cha soka England (FA) ilitoa taarifa watafanya uchunguzi baada ya tukio hilo la shabiki la kumpiga Ramsdale. Chanzo cha tukio hilo ni hasira za mashabiki wa Tottenham baada ya Ramsdale kuwabeza mchezo huo ulipomalizka.

Tukio hilio liliambatana na fujo huku mashabiki wa Tottenham wakirusha chupa za maji uwanjani kabla ya Joseph hajapanda uzio wa uwanja ma kumrukia Ramsdale. Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ilimbidi aingie uwanjani kuwatuliza wachezaji wake na kuwatoa nje akiwemo Granit Xhaka.

Taarifa iliyotolewa na FA iliandika wanatambua tukio zima lilitokea na uchunguzi ulifanyika kubaini chanzo kizima, vile vile chama hicho kimekemea vitendo vya kihalifu na hatua kali itachukuliwa. "Tunakemea tabia ya shabiki huyo baada ya tukio hilo, matukio ya utovu wa nidhamu hayakubaliki, polisi watafanya uchunguzi baada ya kushirikishwa, klabu ya Arsenal imeangalia tukio zima kwenye video ili wamtambue shabiki huyo"

Tukio kama hilo sio mara ya kwanza kutokea, mwaka 2019 shabiki wa Birmingham alifungwa jela baada ya kumsukuma Jack Grealish kipindi anakipiga Aston Villa, tukio hilo limetokea kwenye mechi ya Kombe la FA, shabiki mwingine alifungwa jela kwa muda wa miezi minne baada ya kuwachapa ngumi wachezaji wawili wa Nottingham Forest kwenye mechi nyingine ya Kombe la FA.

Ramsdale alielezea tukio zima baada ya mchezo huo "Mashabiki wa Spurs ndio walianza kuzomea, mimi nikawarudishia kwa kebehi, inashangaza mambo kama haya yanatokea kwenye soka, nashukuru hakuna kitu kilichonitokea,"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live