Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FA kumpa Timu ya England Pep Guardiola

Pep Guardiola.jpeg Pep Guardiola

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha soka la England (FA) kimeripotiwa kuangalia uwezekano wa kuteua kocha wa mpito wa kuchukua nafasi ya Gareth Southgate ili mamlaka hiyo ya soka ijaribu kumshawishi Pep Guardiola aje kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England.

Wakati jambo hilo bado halijathibitishwa, Mail Sport inafahamu kuwa Guardiola anatarajiwa kuondoka Manchester City wakati mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu ujao, akiwa ameiwezesha timu hiyo ya wananchi kushinda mataji 15 makubwa, likiwamo kombe lao la kwanza katika historia ya klabu la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Jina lake limetajwa kwenye orodha ya makocha kadhaa wa kumrithi Southgate, ambaye alijiuzulu nafasi yake ya ukocha wa timu ya taifa ya England Jumanne, baada ya kuiongoza timu hiyo kwa miaka minane.

Kwa mujibu wa The Independent, ‘mabosi wa FA wako tayari kumsubiri Guardiola' na wakati ikiwa si dhamira yao kumtaka aondoke Man City mara moja, kocha huyo ‘Mhispaniola ndiye kocha anayevutia zaidi' kupewa nafasi hiyo ya kuifundisha hivyo wako tayari kuteua kocha wa mpito ili kumsubiri Pep.

Mkataba wa Southgate na England ulikuwa umalizike Desemba na maswali yalikuwa yakiongezeka kama kocha huyo wa Three Lions angeendelea kubaki madarakani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live