Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eymael awatuliza mashabiki

A083577dd55135c9c1a4fb227330d59f.png Yanga na Azam

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa Yanga, Luc Eymael amesema kutolewa katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kufungwa mabao 4-1 dhidi ya watani zao wa jadi Simba isiwe ni sababu ya kuwakatisha tamaa mashabiki.

Eymael aliyasema hayo Dar es Salaam juzi baada ya kumalizika kwa mechi ya Yanga dhidi ya Singida United uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Alisema hata kama wangefungwa mabao 2-1 au 3-1 kwa vyovyote wangekuwa wametolewa katika michuano hiyo na wakati mwingine hutokea kufungwa hivyo.

Alitolea mfano Liverpool iliwahi kufungwa na Manchester City mabao 4-0 na kuendelea lakini haikuwafanya mashabiki wake kukata tamaa na kushindwa kwenda uwanjani.

“Haijalishi umefungwa mangapi, kufungwa ni kufungwa, tunatakiwa kuangalia nini kilitokea kwa sababu wakati mwingine hutokea, na kurudi tena kujipanga,” alisema.

Alisema mchezo wa Jumapili dhidi ya Simba siyo tu walipoteza mechi bali, pesa, mashabiki na vitu mbalimbali lakini wanajaribu kusahau na kurejea tena na hatimaye wachezaji wamejitahidi na kupata ushindi dhidi ya Singida.

Katika mchezo dhidi ya Singida alisema walikuwa na uwezo wa kuibuka ushindi wa zaidi ya mabao sita kutokana na nafasi nyingi walipata. Ushindi huo umeifanya Yanga kupanda hadi ya pili na kufikisha pointi 67 na Azam ikishuka nafasi ya tatu baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa na kubaki na pointi 65.

Kocha wa Singida, Ramadhan Nsanzurwimo alisema timu yake licha ya kushuka daraja walicheza kwa kiwango kizuri. Alisema kufanya kwao vibaya msimu huu kumetokana na mengi na wamekuja kushtuka tayari muda ulikuwa umekwenda.

Nsanzurwimo alisema kama viongozi wa klabu hiyo hawatakaa pamoja na kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza mwakani basi hata yeye hatoweza kusalia hapo. Singida inashika mkia ikiwa na pointi 15 katika michezo 35 iliyocheza ikiwa timu ya kwanza kutangulia kushuka msimu huu.

Chanzo: habarileo.co.tz