Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Exclusive: Pacome aumia kabla ya kuwavaa Waarabu, Avic Town kama msiba!

Pacome Day Insta Pacome Zouzoua.

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imefahamika kuwa, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga raia wa Ivory Coast, Pacome Zouzoua aliumia mazoezini siku ya Ijumaa ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wao wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa Habari wa Kikosi cha Yanga, Ally Kamwe wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo wao wa mwisho wa makundi dhidi ya Al Ahly.

Licha ya kuumia, Pacome ambaye ilikuwa ni siku yake 'Pacome Day' alikomaa na kucheza mchezo huo ambao alionesha kiwango bora na kuisaidia timu yake kushinda bao 4-0 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

“Mchezaji wetu, Pacome Zouzoua, Ijumaa ambapo ni siku moja kabla ya mchezo aliumia mazoezini, haku-train. Aliingia mazoezini dakika mbili tu wakati anapiga mpira akashitua mguu wake, akaumia akakaa palepale. Alibebwa akatolewa nje, akaanza kulia na pale Avic Town pakawa kama msiba vile.

“Tliambizana habari hii isitoke kwa sababu wapo watu watafurahia hili jambo na kuliongezea dua, tutawapa simanzi mashabiki zetu ambao wamejiandaa wiki nzima kwa ajili ya hili jambo. Ijumaa, Pacome alionesha dalili za kutokucheza, Mungu ni mwingi wa rehema.

“usiku ule, Pacome akamwambia daktari wetu kwamba hata kama ikibidi, hii mechi iwe mchezo wangu wa mwisho kwenye maisha yangu kwa ajili ya heshima ambayo Wanayanga wamenipatia. Hata ikibidi niinuke na mguu mmoja, huu mwingine muukate, nitacheza.

“Pacome siku ya Jumamosi anaamka, wakati anakwenda kugongewa chumbani watu wanasubiri habari mbaya kwamba hatocheza akamwambia daktari nimo, najisikia vizuri wewe ongeza barafu, akapigwa barafu akapewa na dawa za maumivu.

“Wakati kocha anapanga kikosi akamuuliza vipi, akasema kama nafaa kupnangwa nipange nimo, hii asilimia 50 ya hali yangu inanitosha kucheza, hii ni siku yangu na ninakwenda kucheza kwa ajili ya mapenzi waliyonionesha Wanayanga, alichokifanya mnakijua.

“Kama mnakumbuka, kipindi cha kwanza kuna wakati alikuwa anacheza kisha anasimama, anaimana kidogo, alikuwa na maumivu makali kweli lakini kwa sababu alikuwa na mapenzi makubwa na mashabiki alifanya kazi kweli.

“Kama aliweza kucheza akiwa na asilimia 50 tu ya fitness level yake huku anachechemea, vipi angekuwa fit asimilia 100? Waarabu wangekunjana sana mashati mno siku hiyo," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live