Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#Exclusive; Mo Dewji: Nimemsamehe Manara, nipo tayari kufanya naye kazi

Manara Mo Dewji Mo Dewji na Haji Manara

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Heshima wa Klabu ya Yanga, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ amesema kuwa amemsamehe aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara kufuatia matusi ambayo amekuwa akimtukana mitandaoni baada ya kuondoka katika klabu hiyo.

Mo Dewji ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na Global TV Online kuhusu adha anayoipata kufuatia kauli za Manara kuhusu Mo Dewji na viongozi wa Simba kwa ujumla.

“Huyu ndugu yetu tumefanya naye kazi vizuri, najua amekuwa akinitukana na ananitukana lakini mimi nimemsamahe kwa sababu maisha ni mafupi, hayo yamepita hata kama akiendelea kunitukana mimi nimemsamehe.

“Na si yeye tu, kuna wengine pia ambao wamenisema vibaya, na kunitukana. Mimi ni aina ya mtu ambaye siweki chuki ndani ya moyo wangu. Mungu amenijalia vitu viwili, kwanza sina wivu na mtu na pili sibaki na kinyongo, likitokea jambo mimi nasamehe na ninamwachia Mungu.

“Ikitokea siku moja amekuja kuomba msamaha mimi kusema ukweli sikuwa na shida na Haji Manara, tumetofautiana kwenye maono, kwenye shabaha ya Simba, hapo ndipo tulipoishia. Mimi sina shida naye, tayari nishamsamehe na kunitukana kwangu wala hainipi shida yoyote.,” amesema Mo Dewji.

Ikumbukwe kuwa, mwishoni mwa msimu wa mwaka 2020/2021 Haji Manara aliondoka Simba na kujiunga na Yanga kwa kile alichodai kuwa ni kutofautiana na baadhi ya viongozi wa Simba ambao walimtuhumu kuihujumu klabu hiyo huku akidai kudukuliwa mawasiliano yake ya simu kinyume cha sheria.

Hata hivyo, ilielezwa kuwa, baadhi ya viongozi hao hawakutaka afanye kazi za matangazo na wadhamini wa Yanga, GSM huku vyanzo vingine vikidai kuwa mshahara aliokuwa akilipwa klabuni hapo ulikuwa mdogo ikilinganishwa na kazi aliyokuwa akiifanya.

Baada ya kuondoka Simba na kujiunga na Yanga, Manara amekuwa akiwatuhumu viongozi hao akiwemo o na Barbara (aliyekuwa CEO wa Simba) kwa madai kuwa hawakutaka aendelee kuitumikia Simba na kwamba alifanyiwa mambo mengi ya hovyo ili aondoke klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live