Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ex wake kocha Eriksson aangua kilio kwenye TV

Sven Goran Ex wake kocha Eriksson aangua kilio kwenye TV

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa patna wa kocha Sven-Goran Eriksson, mrembo Nancy Dell'Olio ameangua kilio akiwa mubashara kwenye televisheni baada ya kufichua mazungumzo yao ya mwisho aliyozungumza na mpenzi wake huyo kabla ya kufariki dunia mapema wiki hii.

Eriksson, aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya England alifariki dunia kwa maradhi ya saratani ya kongosho akiwa na umri wa miaka 76.

Mrembo Nancy, 63, alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Eriksson kwa miaka 10 kabla ya kuachana 2007.

Mrembo huyo alihojiwa kwenye kipindi cha televisheni cha Good Morning Britain, ambapo alishindwa kuzuia hisia zake na kuangua kilio wakati alipokuwa akifichua mazungumzo yao ya mwisho waliyofanya siku chache kabla hajafariki.

Nancy aliambia GMB: "Ninachoweza kusema alikuwa anajaribu kujionyesha kwamba yupo vizuri kwenye mazungumzo ya simu na muda mwingine alikuwa hapokei simu. Sikuwahi kuwaza kwamba atakufa. Siku zote niliamini kunaweza kuwa na muujiza."

Mtangazaji wa GMB, Richard Madeley alilazimika kumwomba msamaha Nancy baada ya mrembo huyo kushindwa kuendelea na mazungumzo. Mrembo alisema alikuwa akiwasiliana na Eriksson kwa muda wote wa ugonjwa wake.

Alisema muda wote Eriksson alionekama hana shida na alikuwa akicheka kumfanya asiwe na wasiwasi, aliposema: "Ilikuwa ngumu sana, lakini alikuwa anaonekana kutokuwa na wasiwasi na tulikuwa tunacheka na kama alikuwa akisema 'najisikia vizuri'.

"Ilikuwa ngumu sana kuizungumzia hiyo, lakini nilijaribu kujikaza na kusubiri kuona itakavyokuwa. Nilitaka tukutane kwa ajili ya mlo wa jioni."

Sven-Goran Eriksson alijirekodi video ya kuaga na kutoa ujumbe ambao uliwaliza waliokuwa wakimrekodi. Baada ya kifo cha Eriksson, mrembo Nancy aliposti picha zake alizokuwa na kocha huyo kipindi walipokuwa wakifurahia maisha wakati wa uhusiano wao.

Mrembo Nancy alikiri kwamba bado alikuwa anampenda Eriksson kwa sababu alikuwa mtu safi. Nancy alikuwa mke wa Giancarlo Massa wakati anakutana na Eriksson kwa mara ya kwanza na jambo hilo lilimfanya avunje uhusiano wake na mumewe ili awe na kocha huyo raia wa Sweden.

Wawili hao hawakufunga ndoa, lakini mara zote mrembo Nancy alizomzungumzia Eriksson alikuwa akimtambua kama mumewe wa zamani.

Uhusiano wao wa kimapenzi ulitibuka baada ya kugundulika kwamba Eriksson alikuwa kwenye uhusiano wa siri na mrembo wa Sweden, Ulrika Jonsson mwaka 2002. Miaka miwili badaaye, Eriksson aliangukia tena kwenye penzi la mtu mwingine na safari hii ilikuwa na sekretari wa Chama cha Soka England, mrembo Faria Alam. Huko nyuma, Eriksson alikuwa ameoana na mrembo Ann-Christine Pettersson kabla ya kukutana na Nancy.

Ndoa hiyo ilidumu kati ya mwaka 1977 na 1994. Sven mwenyewe aliwahi kufichua ndoa yake ilikufa baada ya kuwa na uhusiano na mrembo Graziella Mancinelli.

Chanzo: Mwanaspoti