Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ex wa Antony afunguka alivyoshambuliwa mpaka mimba kuharibika

Gabriela Cavallin Ex wa Antony afunguka alivyoshambuliwa mpaka mimba kuharibika

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gabriela Cavallin, mpenzi wa zamani wa Antony amezungumzia zaidi tuhuma za unyanyasaji wa nyumbani na vitisho vya kifo dhidi ya winga huyo wa Manchester United.

Katika mahojiano ya runinga na chombo cha habari Ureno cha UOL Esporte,

"Alinishambulia, akanisukuma kwenye mlango (wa gari). Hapo, nilijiambia: 'Imekwisha,'" Mshawishi na DJ huyo alisema.

Takriban wiki mbili zilizopita, ripoti ziliibuka kuwa Bi Cavallin alikuwa amemshutumu winga huyo wa miaka 23 kwa unyanyasaji wa nyumbani, vitisho na majeraha ya mwili na alikuwa amefungua kesi dhidi yake nchini Brazil.

Ripoti za awali zilieleza kuwa inadaiwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 alishambuliwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mnamo Mei 20 mwaka huu, siku ambayo nyota huyo wa zamani wa Ajax alipochezea Man United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Bournemouth kwenye Uwanja wa Vitality. Pia zilielezea madai mengi, ambayo baadhi yalifanyika katika klabu ya usiku jijini Sao Paulo mwezi Julai 2022 na matukio zaidi yanayodaiwa kutokea nchini Uingereza.

Bi Cavallin pia anamshutumu Antony kwa kumfanya mfungwa wake nyumbani kwao peke yake na kutomruhusu kuondoka.

"Alivunja briefcase yangu, akachukua mkoba wangu, karatasi zangu za kusafiria, alivunja simu yangu, hakuniruhusu niondoke. Nilikuwa mfungwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tisa unusu asubuhi, nakiita kifungo cha faragha. Nilitaka tu kutoka nje na akaniambia kuwa sitaondoka mpaka nifute kila kitu. Nafikiri mama yake alimpigia simu physiotherapist na kuomba msaada. Hakuna angeweza kudhibiti."

Wakati wa mahojiano, Bi Cavallin pia alifichua kuwa alipoteza ujauzito, jambo ambalo alisema lilimvunja moyo sana.

"Ilikuwa huzuni kubwa zaidi ya maisha yangu na pia hisia ya hatia kubwa zaidi. Wakati huo, nilikufa. Niliogopa, nilianza kulia sana."

Cavallin anadai kuwa alikuwa mwathirika wa ghasia alipokuwa amebeba mtoto wao tumboni. Tukio hilo linasemekana kutokea wakati wanandoa hao wakiishi Amsterdam wakati Antony alikuwa bado anaichezea Ajax.

"Alikuwa amerudi kutoka likizo na kunipigia simu. Alikuwa anaomba msamaha tu, akisema anajuta sana kwa kilichotokea,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: