Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ex wa Anthony aitaka Man United imsimamishe mchezaji huyo

 Xlarge.png Ex wa Anthony aitaka Man United imsimamishe mchezaji huyo

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpenzi wa zamani wa Antony, Gabriela Cavallin kuhusu taarifa rasmi ya Manchester United:

“Kwa nini iliichukua United miezi mitatu? Sio sawa. Ninapendelea kutoamini kuwa klabu kubwa kama hii, yenye watu makini na wenye taaluma, inaweza kuficha hali kama hii.”

“Antony lazima aondolewe uwanjani (asiruhusiwe kucheza). Inasikitisha kwamba bado ameruhusiwa kucheza huku uchunguzi ukiendelea.”

“Nimesikitishwa kabisa na mchakato huu wote. Maisha yanawezaje kuendelea kama kawaida kwake? Hawawezi kujua wanachojua sasa na kutofanya lolote. Anapaswa kusimamishwa kazi.”

“Sitakata tamaa. Watu wanatakiwa kuwajibika. Haijalishi ni taaluma gani au mtu anaweza kuwa maarufu kiasi gani. Ikiwa walichukua hatua dhidi ya mwenzake, sioni kwa nini Antony achukuliwe tofauti”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live