Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Everton yapunguziwa pointi mbili kwa kukiuka kwa mara ya pili

Everton Yapunguziwa Pointi Mbili Kwa Kukiuka Kwa Mara Ya Pili Everton yapunguziwa pointi mbili kwa kukiuka kwa mara ya pili

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Everton wamepokonywa pointi mbili kwa kukiuka mara ya pili kanuni za fedha za Premier League.

Sheria za faida na uendelevu (PSR) ziliruhusu vilabu kupoteza pauni milioni 105 kwa miaka mitatu na tume huru ilipata Everton imekiuka hilo kwa pauni milioni 16.6 kwa kipindi cha miaka mitatu hadi 2022-23.

Wanashuka nafasi moja hadi ya 16 na sasa wako pointi mbili juu ya eneo la kushushwa daraja.

Toffees ilipunguziwa pointi 10 hadi sita baada ya kukata rufaa mwezi Februari kwa kipindi cha miaka mitatu hadi 2021-22.

Everton imesema klabu hiyo itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Katika sababu zake zilizoandikwa tume huru ilikubali hoja za klabu za kupunguza kuhusiana na ukweli ambao klabu:

Tayari imepunguziwa pointi msimu huu Kupoteza mapato ya klabu kwa sababu ya kusitishwa kwa mkataba wa udhamini na kampuni ya Urusi ya USM Kukiri hatia mapema

Chanzo: Bbc