Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Everton yamvutia waya Rooney

Evatton Pic Wayne Rooney

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Huenda Wayne Rooney akapewa nafasi ya kuwa kocha wa Everton kwa mara nyingine akichukua nafasi ya Frank Lampard anayesuasua Ligi Kuu England kwasasa.

Taarifa zimeripoti Rooney amepigiwa debe na mwenyekiti wa klabu hiyo Farhad Moshiri kwasababu yupo kwenye orodha ya makocha wanaowania nafasi ya ukocha Everton.

Lampard alipokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Brighton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England wikiendi iliyopita na kukalia kutia taarifa zikiripoti huenda akafungashiwa virago.

Everton ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi baada ya kukusanya pointi 15, halafu leo wana kibarua kigumu dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa Kombe la FA.

 Rooney, aliwahi kuichezea Everton mara mbili kipindi anacheza soka anaunga na Roberto Martinez aliyeitema timu ya taifa Ubelgiji baada ya kuboronga kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika Qatar mwezi uliopita. Martinez ndio kocha wa kwanza aliyefungashiwa virago na Moshiri baada ya kuteuliwa mwaka 2016, katika makocha watano waliotimuliwa na bosi huyo.

Makocha wengine waliopo kwenye orodha hiyo ni kocha wa zamani wa Burnley, Sean Dych na kocha anayefundisha Celtic, Ange Postecoglu are other options.

Aidha kwasasa Rooney anainoa DC United kutoka Marekani lakini bosi wa Everton, Bushiru anaamini Rooney atakuwa tu sahihi kwasababu anaifahamu vizuri klabu hiyo kwa muda mrefu. Kabla ya kutua DC United, Rooney alikuwa akiinoa Derby County.

Kwasasa Lampard anapigania nafasi yake kibarua chake kisiote nyasi baada ya mashabiki wa Everton kucharuka. Imeelezwa Lampard atakiongoza kikosi chake dhidi ya Man United kwenye mechi ya Kombe la FA.

Chanzo: Mwanaspoti